Acts 10:28
Akawaambia, “Mnajua kabisa kwamba ni kinyume cha sheria yetu Myahudi kuchangamana na mtu wa Mataifa au kumtembelea. Lakini Mungu amenionyesha kwamba nisimwite mtu yeyote kuwa najisi au asiye safi.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
27Petro alipokuwa akizungumza naye akaingia ndani na kukuta watu wengi wamekusanyika.
Cross References
Isaiah 65:5wasemao, ‘Kaa mbali; usinikaribie, 2 kwa maana mimi ni mtakatifu mno kwako!’ 1 Watu wa aina hiyo ni moshi katika pua zangu, 2 ni moto uwakao mchana kutwa. 1
John 4:9Yule mwanamke Msamaria akamjibu, “Wewe ni Myahudi na mimi ni Msamaria. Yawezekanaje uniombe nikupe maji ya kunywa?” (Wayahudi walikuwa hawashirikiani kabisa na Wasamaria.)
John 18:28Ndipo Wayahudi wakamchukua Yesu kutoka kwa Kayafa na kumpeleka kwenye jumba la kifalme la mtawala wa Kirumi. + 18:28 Jumba la mfalme la mtawala wa Kirumi lilikuwa linaitwa Praitorio. Wakati huo ilikuwa ni alfajiri, ili kuepuka kuwa najisi kwa taratibu za ibada, Wayahudi hawakuingia ndani kwa sababu ya sheria za Kiyahudi. Wangehesabiwa kuwa najisi kama wangeingia nyumbani mwa mtu asiye Myahudi na wasingeruhusiwa kushiriki katika Sikukuu ya Pasaka.
Acts 10:34Ndipo Petro akafungua kinywa chake akasema, “Mungu hana upendeleo,
Acts 11:9“Sauti ikasema kutoka mbinguni mara ya pili, ‘Usikiite najisi kitu chochote Mungu alichokitakasa.’
Acts 22:21“Ndipo Bwana akaniambia, ‘Nenda, kwa maana nitakutuma mbali, kwa watu wa Mataifa.’ ” 1 Paulo Na Jemadari Wa Kirumi