Acts 13:34
Kwa kuwa Mungu alimfufua kutoka kwa wafu asioze kamwe, alitamka maneno haya: 1 “ ‘Nitakupa wewe baraka takatifu zilizo za hakika 2 nilizomwahidi Daudi.’
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
2 Samuel 7:14Nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu. Atakapokosea nitamwadhibu kwa fimbo ya wanadamu, kwa adhabu ya kupigwa na wanadamu.
Psalms 89:2Nitatangaza kuwa upendo wako unasimama imara milele 2 na uaminifu wako umeuthibitisha mbinguni. 1
Isaiah 55:3Tegeni sikio mje kwangu, 2 nisikieni mimi, ili nafsi zenu zipate kuishi. 1 Nitafanya agano la milele nanyi, 2 pendo la uaminifu nililomwahidi Daudi. 1
Jeremiah 33:26basi nitawakataa wazao wa Yakobo na Daudi mtumishi wangu, na sitachagua mmoja wa wanawe kutawala juu ya wazao wa Abrahamu, Isaki na Yakobo. Kwa maana nitawarudisha kutoka nchi ya kutekwa kwao na kuwaonea huruma.’ ”
Ezekiel 37:24“ ‘Mtumishi wangu Daudi atakuwa mfalme juu yao, nao wote watakuwa na mchungaji mmoja. Watafuata sheria zangu na kuzishika amri zangu kwa uangalifu.
Amos 9:11“Katika siku ile nitaisimamisha 2 hema ya Daudi iliyoanguka. 1 Nitakarabati mahali palipobomoka 2 na kujenga upya magofu yake, 2 na kuijenga kama ilivyokuwa awali, 1