Acts 17:5
Lakini Wayahudi ambao hawakuwa wameamini wakawa na wivu, wakawakodi watu waovu kutoka sokoni, wakakutanisha umati wa watu, wakaanzisha ghasia mjini. Wakaenda mbio nyumbani kwa Yasoni wakiwatafuta Paulo na Sila ili kuwaleta nje penye ule umati wa watu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Job 30:1“Lakini sasa watu wadogo kwa umri kuniliko wananidhihaki, 1 watu ambao baba zao ningekataa kwa dharau 2 kuwaweka pamoja na mbwa wangu wa kulinda kondoo. 1
Psalms 69:12Wale wanaoketi mlangoni wananisimanga, 2 nimekuwa wimbo wa walevi. 1
Isaiah 26:11Ee Bwana, mkono wako umeinuliwa juu, 2 lakini hawauoni. 1 Wao na waone wivu wako kwa ajili ya watu wako tena waaibishwe, 2 moto uliowekwa akiba kwa ajili ya adui zako na uwateketeze. 1
Acts 7:9“Kwa sababu wazee wetu walimwonea wivu Yosefu ndugu yao, walimuuza kama mtumwa huko Misri. Lakini Mungu alikuwa pamoja naye.
Acts 14:2Lakini wale Wayahudi waliokataa kuamini, wakawachochea watu wa Mataifa, wakatia chuki ndani ya mioyo yao dhidi ya wale walioamini.
Acts 17:7naye Yasoni amewakaribisha nyumbani mwake. Hawa wote wanaasi amri za Kaisari wakisema yuko mfalme mwingine aitwaye Yesu.”