Acts 2:33
Basi ikiwa yeye ametukuzwa kwa mkono wa kuume wa Mungu, amepokea kutoka kwa Baba ahadi ya Roho Mtakatifu, naye amemimina kile mnachoona sasa na kusikia.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
32Mungu alimfufua huyu Yesu na sisi sote ni mashahidi wa jambo hilo.
Cross References
Psalms 89:24Upendo wangu mkamilifu utakuwa pamoja naye, 2 kwa Jina langu pembe yake itatukuzwa. 1
Psalms 118:22Jiwe walilolikataa waashi, 2 limekuwa jiwe kuu la pembeni. 1
Isaiah 53:12Kwa hiyo nitamgawia sehemu miongoni mwa wakuu, 2 naye atagawana nyara pamoja na wenye nguvu, 1 kwa sababu aliyamimina maisha yake hadi mauti, 2 naye alihesabiwa pamoja na wakosaji. 1 Kwa kuwa alichukua dhambi za wengi, 2 na kuwaombea wakosaji.
Mark 16:19Baada ya Bwana Yesu kusema nao, alichukuliwa juu mbinguni na kuketi mkono wa kuume wa Mungu.
John 7:38Yeyote aniaminiye mimi, kama Maandiko yasemavyo, vijito vya maji ya uzima vitatiririka ndani mwake.”
John 14:26Lakini huyo Msaidizi, yaani, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwenu kwa Jina langu, atawafundisha mambo yote na kuwakumbusha yote niliyowaambia.