Amos 7:17
“Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana: 1 “ ‘Mke wako atakuwa kahaba mjini, 2 nao wana wako na binti zako watauawa kwa upanga. 1 Shamba lako litapimwa na kugawanywa, 2 na wewe mwenyewe utafia katika nchi ya kipagani. 1 Nayo Israeli kwa hakika itakwenda uhamishoni, 2 mbali na nchi yao.’ ”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
2 Kings 17:6Katika mwaka wa tisa wa Hoshea, mfalme wa Ashuru akaiteka Samaria na kuwahamishia Waisraeli huko Ashuru. Akawaweka huko Hala, na Gozani karibu na Mto Habori, na katika miji ya Wamedi. 1 Israeli Inakwenda Uhamishoni Kwa Sababu Ya Dhambi
Isaiah 13:16Watoto wao wachanga watavunjwa vipande vipande 2 mbele ya macho yao; 1 nyumba zao zitatekwa 2 na wake zao watatendwa jeuri. 1
Jeremiah 20:6Nawe Pashuri pamoja na wote waishio katika nyumba yako mtakwenda uhamishoni Babeli. Mtafia humo na kuzikwa, wewe na rafiki zako wote ambao umewatabiria uongo.’ ” 1 Malalamiko Ya Yeremia 1
Jeremiah 28:16Kwa hiyo, hili ndilo asemalo Bwana: ‘Hivi karibuni nitakuondoa kutoka juu ya uso wa dunia. Mwaka huu utakufa, kwa sababu umetangaza uasi dhidi ya Bwana.’ ”
Jeremiah 29:25“Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: Ulituma barua kwa jina lako mwenyewe kwa watu wote wa Yerusalemu, kwa Sefania mwana wa kuhani Maaseya na kwa makuhani wengine wote. Ulimwambia Sefania,
Jeremiah 29:32hili ndilo Bwana asemalo: Hakika nitamwadhibu Shemaya Mnehelami pamoja na uzao wake. Hapatakuwa na yeyote atakayebaki miongoni mwa watu hawa, wala hataona mema nitakayowatendea watu wangu, asema Bwana, kwa sababu ametangaza uasi dhidi yangu.’ ”