Daniel 11:4
Baada ya kujitokeza, milki yake itavunjwa na kugawanyika katika pande nne za mbinguni. Hautakwenda kwa wazao wake, wala hautakuwa na nguvu alizotumia, kwa sababu milki yake itangʼolewa na kupewa wengine.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
3Ndipo mfalme mwenye nguvu atatokea, ambaye atatawala kwa nguvu nyingi na kufanya anavyopenda.
Cross References
Job 20:5macheko ya mtu mwovu ni ya muda mfupi, 2 nayo furaha ya wasiomcha Mungu hudumu kwa kitambo tu. 1
Psalms 39:6Hakika kila binadamu ni kama njozi 2 aendapo huku na huko: 1 hujishughulisha na mengi lakini ni ubatili; 2 anakusanya mali nyingi, 2 wala hajui ni nani atakayeifaidi. 1
Psalms 73:17Mpaka nilipoingia patakatifu pa Mungu, 2 ndipo nilipotambua mwisho wao. 1
Ecclesiastes 4:8Kulikuwepo mwanadamu aliye peke yake, 2 hakuwa na mwana wala ndugu. 1 Hapakuwa na mwisho wa kazi yake, 2 hata hivyo macho yake 2 hayakutosheka na utajiri wake. 1 Aliuliza, “Ninajitaabisha hivi kwa ajili ya nani, 2 nami kwa nini ninajinyima kufurahia?” 1 Hili pia ni ubatili, 2 ni shughuli yenye taabu! 1
Jeremiah 12:17Lakini kama taifa lolote halitasikiliza na kutii, nitalingʼoa kabisa na kuliangamiza,” asema Bwana.
Jeremiah 31:40Bonde lote watupwapo maiti na majivu pia na matuta yote kutoka Bonde la Kidroni upande wa mashariki hadi pembe ya Lango la Farasi, itakuwa takatifu kwa Bwana. Kamwe mji huu hautangʼolewa tena wala kubomolewa.”