Daniel 2:34
Ulipokuwa unaangalia, jiwe lilikatwa, lakini si kwa mikono ya mwanadamu. Lile jiwe liliipiga ile sanamu kwenye nyayo zake za chuma na udongo wa mfinyanzi, na kuivunja.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Psalms 110:5Bwana yuko mkono wako wa kuume, 2 atawaponda wafalme siku ya ghadhabu yake. 1
Psalms 149:6Sifa za Mungu na ziwe vinywani mwao 2 na upanga ukatao kuwili mikononi mwao, 1
Isaiah 60:12Kwa maana taifa au ufalme ule ambao hautakutumikia utaangamia; 2 utaharibiwa kabisa. 1
Ezekiel 47:5Akapima tena dhiraa 1,000 nyingine, lakini wakati huu yalikuwa mto ambao sikuweza kuvuka, kwa kuwa maji yalikuwa na kina kirefu ambacho ni cha kuogelea, mto ambao hakuna mtu yeyote ambaye angeweza kuvuka.
Daniel 7:13“Katika maono yangu ya usiku nilitazama, na mbele yangu nikamwona anayefanana na mwanadamu, akija pamoja na mawingu ya mbinguni. Akamkaribia huyo Mzee wa Siku, na akaongozwa mbele zake.
Daniel 8:25Atasababisha udanganyifu ustawi, naye atajihesabu mwenyewe kuwa bora. Wakati wajisikiapo kuwa wako salama, atawaangamiza wengi, na kushindana na Mkuu wa wakuu. Lakini ataangamizwa, isipokuwa si kwa uwezo wa mwanadamu.