Isaya 60:12
Kwa maana taifa au ufalme ule ambao hautakutumikia utaangamia; 2 utaharibiwa kabisa. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Isaiah 14:2Mataifa watawachukua 2 na kuwaleta mahali pao wenyewe. 1 Nayo nyumba ya Israeli itamiliki mataifa 2 kama watumishi na wajakazi katika nchi ya Bwana. 1 Watawafanya watekaji wao kuwa mateka, 2 na kutawala juu ya wale waliowaonea.
Isaiah 54:15Kama mtu yeyote akikushambulia, 2 haitakuwa kwa ruhusa yangu; 1 yeyote akushambuliaye 2 atajisalimisha kwako. 1
Daniel 2:35Ndipo ile chuma, ule udongo wa mfinyanzi, ile shaba, ile fedha na ile dhahabu vikavunjika vipande vipande kwa wakati mmoja, na vikawa kama makapi katika sakafu ya kupuria nafaka wakati wa kiangazi. Upepo ukavipeperusha bila kuacha hata alama. Lakini lile jiwe lililoipiga ile sanamu likawa mlima mkubwa mno na kuijaza dunia yote.
Zechariah 12:2“Nitakwenda kufanya Yerusalemu kuwa kikombe cha kuyumbisha mataifa yote yanayoizunguka. Yuda utazingirwa kwa vita na Yerusalemu pia.
Zechariah 14:17Ikiwa taifa lolote la dunia hawatakwenda Yerusalemu kumwabudu Mfalme, Bwana Mwenye Nguvu Zote, mvua haitanyesha kwao.
Matthew 21:44Yeye aangukaye juu ya jiwe hili atavunjika vipande vipande, lakini yule litakayemwangukia atasagwa kabisa.”