Daniel 2:47
Mfalme akamwambia Danieli, “Hakika Mungu wako ni Mungu wa miungu, na Bwana wa wafalme, na mfunuaji wa siri zote, kwa maana umeweza kufunua siri hii.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 41:39Ndipo Farao akamwambia Yosefu, “Maadamu Mungu amekufunulia yote haya, hakuna mwingine yeyote mwenye akili na hekima kama wewe.
Joshua 22:22“Yeye Mwenye Nguvu, Mungu, Bwana! Yeye Mwenye Nguvu, Mungu, Bwana! Yeye anajua! Israeli na wajue! Kama huu umekuwa ni uasi au kukosa utii kwa Bwana, msituache hai siku hii ya leo.
Job 12:19Huwaondoa makuhani wakiwa wametekwa nyara, 2 na kuwaangusha waliojiimarisha muda mrefu. 1
Psalms 72:11Wafalme wote watamsujudia 2 na mataifa yote yatamtumikia. 1
Psalms 96:4Kwa kuwa Bwana ni mkuu mwenye kustahili kusifiwa kuliko wote; 2 yeye ni wa kuogopwa kuliko miungu yote. 1
Proverbs 8:15Kwa msaada wangu wafalme hutawala 2 na watawala hutunga sheria zilizo za haki, 1