Daniel 5:23
Badala yake, umejiinua dhidi ya Bwana wa mbingu. Uliletewa vikombe vya Hekalu lake, nawe na wakuu wako, wake zako na masuria wako mlivitumia kwa kunywea mvinyo. Ukaisifu miungu ya fedha na dhahabu, ya shaba, chuma, miti na mawe, miungu ambayo haiwezi kuona, au kusikia wala kufahamu. Lakini hukumheshimu Mungu ambaye anaushikilia uhai wako na njia zako zote mkononi mwake.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
22“Lakini wewe mwanawe, ee Belshaza, hukujinyenyekeza, ingawa ulifahamu haya yote.
24Kwa hiyo ameutuma mkono ule ulioandika maneno.
Cross References
Genesis 2:7Bwana Mungu alimuumba mtu kutoka mavumbi + 2:7 Neno la Kiebrania la mavumbi ya ardhi ndilo kiini cha jina Adamu. ya ardhi, akampulizia pumzi ya uhai puani mwake, naye mtu akawa kiumbe hai.
Judges 16:23Basi viongozi wa Wafilisti wakakusanyika pamoja ili kutoa kafara kwa mungu wao Dagoni na kufanya karamu, wakisema, “Mungu wetu amemtia adui yetu Samsoni mikononi mwetu.”
1 Samuel 17:26Daudi akauliza watu waliokuwa wamesimama karibu naye, “Je, atafanyiwa nini mtu atakayemuua huyu Mfilisti na kuondoa aibu hii katika Israeli? Ni nani huyu Mfilisti asiyetahiriwa hata atukane majeshi ya Mungu aliye hai?”
2 Kings 14:10Hakika umeishinda Edomu, na sasa unajivuna. Jisifu katika ushindi wako, lakini kaa nyumbani kwako! Kwa nini unachokoza na kujiletea anguko lako mwenyewe na la Yuda pia?”
Job 31:4Je, yeye hazioni njia zangu 2 na kuihesabu kila hatua yangu? 1
Psalms 104:29Unapoficha uso wako, 2 wanapata hofu, 1 unapoondoa pumzi yao, 2 wanakufa na kurudi mavumbini. 1