Daniel 8:2
Katika maono yangu, nilijiona nikiwa ndani ya ngome ya Shushani katika jimbo la Elamu. Katika maono nilikuwa kando ya Mto Ulai. + 8:2 Mto Ulai ni mfereji uliokuwa kati ya Shushani na Elymaisi; sasa unaitwa Mto Karuni.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 14:1Wakati huu Amrafeli mfalme wa Shinari, Arioko mfalme wa Elasari, Kedorlaoma mfalme wa Elamu, na Tidali mfalme wa Goimu
Nehemiah 1:1Maneno ya Nehemia mwana wa Hakalia: Katika mwezi wa Kisleu + 1:1 Kisleu ni mwezi wa tisa katika kalenda ya Kiyahudi; katika kalenda yetu ni Novemba/Desemba (ona pia Zekaria 7:1). katika mwaka wa ishirini, wakati nilikuwa ngomeni katika jumba la kifalme la Shushani,
Esther 2:8Wakati agizo na amri ya mfalme lilitangazwa, wanawali wengi waliletwa kwenye ngome ya mji wa Shushani na kuwekwa chini ya uangalizi wa Hegai. Pia Esta alipelekwa katika jumba la mfalme na akakabidhiwa Hegai, aliyekuwa mkuu wa nyumba ya wanawake.
Esther 7:6Esta akasema, “Mtesi na adui ni huyu mwovu Hamani.” Hamani alifadhaika mbele ya mfalme na malkia.
Esther 9:11Mfalme aliarifiwa siku iyo hiyo hesabu ya waliouawa katika ngome ya Shushani.
Isaiah 11:11Katika siku hiyo Bwana atanyoosha mkono wake mara ya pili kurudisha mabaki ya watu wake waliosalia kutoka Ashuru, Misri, Pathrosi, + 11:11 Pathrosi ina maana Misri ya Juu. Kushi, Elamu, Babeli, Hamathi na kutoka visiwa vya baharini. 1