Kumbukumbu 29:25
Na jibu litakuwa: “Ni kwa sababu watu hawa waliacha Agano la Bwana, Mungu wa baba zao, Agano alilofanya nao wakati alipowatoa katika nchi ya Misri.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
1 Kings 19:10Akajibu, “Nimeona wivu mwingi kwa ajili ya Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote. Waisraeli wamelikataa Agano lako, wamevunja madhabahu zako na kuwaua manabii wako kwa upanga. Ni mimi, mimi peke yangu, niliyebaki, nao sasa wananitafuta ili waniangamize.”
Isaiah 24:1Tazama, Bwana ataifanya dunia kuwa ukiwa 2 na kuiharibu, 1 naye atauharibu uso wake 2 na kutawanya wakaao ndani yake: 1
Jeremiah 22:8“Watu kutoka mataifa mengi watapitia karibu na mji huu na kuulizana, ‘Kwa nini Bwana amefanya jambo la namna hii juu ya mji huu mkubwa?’
Jeremiah 31:32Halitafanana na agano 2 nililofanya na baba zao 1 wakati nilipowashika mkono 2 kuwaongoza watoke Misri, 1 kwa sababu walivunja agano langu, 2 ijapokuwa nilikuwa mume kwao,” 4 asema Bwana. 1
Jeremiah 44:3kwa sababu ya uovu waliokuwa wameufanya. Walinikasirisha kwa kufukiza uvumba na kwa kuabudu miungu mingine ambayo kamwe wao, wala ninyi, wala baba zenu hawakuifahamu.
Hebrews 8:9Agano langu halitakuwa kama lile 2 nililofanya na baba zao 1 nilipowashika mkono 2 kuwaongoza watoke nchi ya Misri, 1 kwa sababu hawakuendelea kuwa waaminifu katika agano langu, 2 nami nikawaacha, 4 asema Bwana. 1