Waebrania 8:9
Agano langu halitakuwa kama lile 2 nililofanya na baba zao 1 nilipowashika mkono 2 kuwaongoza watoke nchi ya Misri, 1 kwa sababu hawakuendelea kuwa waaminifu katika agano langu, 2 nami nikawaacha, 4 asema Bwana. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 19:16Alipositasita, wale watu wakamshika mkono wake na mikono ya mke wake na binti zake wawili na kuwaongoza salama nje ya mji, kwa kuwa Bwana alikuwa na huruma kwao.
Exodus 24:3Mose alipokwenda na kuwaambia watu maneno yote na sheria zote za Bwana, wakaitikia kwa sauti moja, “Kila kitu alichosema Bwana tutakifanya.”
Exodus 34:10Kisha Bwana akasema: “Tazama ninafanya Agano mbele ya watu wako wote. Mbele ya watu wako wote nitafanya maajabu ambayo hayajafanyika katika taifa lolote katika ulimwengu wote. Watu wale mnaoishi miongoni mwao wataona jinsi ilivyo ya kushangaza ile kazi nitakayowafanyia mimi Bwana wenu.
Deuteronomy 5:2Bwana Mungu wetu alifanya Agano nasi katika mlima wa Horebu.
Deuteronomy 29:12Mnasimama hapa ili kufanya Agano na Bwana Mungu wenu, Agano ambalo Mungu analifanya nanyi siku hii ya leo na kulitia muhuri kwa kiapo,
Deuteronomy 31:16Kisha Bwana akamwambia Mose: “Unakwenda kupumzika na baba zako, nao watu hawa hivi karibuni watazini na miungu migeni ya nchi wanayoingia. Wataniacha na kuvunja Agano nililofanya nao.