Esta 1:12
Lakini wakati watumishi walipotoa amri ya mfalme, Malkia Vashti alikataa kuja. Ndipo mfalme alighadhibika, na hasira yake ikawaka.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 32:19Mose alipoikaribia kambi na kuona yule ndama na ile michezo, hasira yake ikawaka, akatupa vile vibao vilivyokuwa mikononi mwake, akavipasua vipande vipande pale chini ya mlima.
Deuteronomy 29:20Bwana kamwe hatakuwa radhi kumsamehe, ghadhabu na wivu wa Mungu vitawaka dhidi ya mtu huyo. Laana zote zilizoandikwa katika kitabu hiki zitamwangukia na Bwana atafuta jina lake chini ya mbingu.
Psalms 79:5Hata lini, Ee Bwana? Je, wewe utakasirika milele? 2 Wivu wako utawaka kama moto hadi lini? 1
Proverbs 20:2Ghadhabu ya mfalme ni kama ngurumo ya simba; 2 yeye amkasirishaye hupoteza uhai wake. 1
Daniel 3:13Mfalme Nebukadneza, akiwa amekasirika na mwenye ghadhabu kali, akawaita Shadraki, Meshaki na Abednego. Hivyo watu hawa wakaletwa mbele ya mfalme,
Nahum 1:6Ni nani awezaye kuzuia hasira yake yenye uchungu? 2 Nani awezaye kuvumilia hasira yake kali? 1 Ghadhabu yake imemiminwa kama moto, 2 na miamba inapasuka mbele zake. 1