Kutoka 10:21
Kisha Bwana akamwambia Mose, “Nyoosha mkono wako kuelekea angani ili giza litande katika nchi ya Misri, giza ambalo watu wanaweza kulipapasa na kulihisi.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 9:22Ndipo Bwana akamwambia Mose, “Nyoosha mkono wako kuelekea angani ili kwamba mvua ya mawe inyeshe juu ya Misri yote, juu ya watu, wanyama na juu ya kila kitu kiotacho katika mashamba ya Misri.”
Deuteronomy 4:34Je, kuna mungu yeyote amepata kujaribu mwenyewe kuchukua taifa moja kutoka taifa lingine, kwa mapigo, kwa ishara za miujiza na maajabu, kwa vita, kwa mkono wenye nguvu na mkono ulionyooshwa au kwa matendo makuu ya kutisha, kama yale ambayo Bwana Mungu wenu aliyofanya kwa ajili yenu huko Misri mbele ya macho yenu?
Job 5:14Giza huwapata wakati wa mchana; 2 wakati wa adhuhuri hupapasa kama vile usiku. 1
Psalms 78:49Aliwafungulia hasira yake kali, 2 ghadhabu yake, hasira na uadui, 2 na kundi la malaika wa kuharibu. 1
Proverbs 4:19Lakini njia ya waovu ni kama giza nene; 2 hawajui kinachowafanya wajikwae. 1
Ecclesiastes 6:4Kuzaliwa kwake hakuna maana, huondokea gizani na gizani jina lake hufunikwa.