Exodus 33:5
Kwa kuwa Bwana alikuwa amemwambia Mose, “Waambie Waisraeli, ‘Ninyi ni watu wenye shingo ngumu. Kama ningefuatana nanyi hata kwa muda mfupi, ningewaangamiza. Sasa vueni mapambo yenu, nami nitaamua nitakalowatendea.’ ”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
4Watu waliposikia habari hizo za huzuni, wakaanza kuomboleza wala hakuna mtu aliyevaa mapambo yoyote.
6Hivyo Waisraeli wakavua mapambo yao katika Mlima wa Horebu. 1 Hema La Kukutania
Cross References
Genesis 22:12Akamwambia, “Usimdhuru kijana, wala usimtendee jambo lolote. Sasa ninajua kwamba unamcha Mungu, kwa sababu hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee.”
Exodus 33:3Pandeni mwende katika nchi itiririkayo maziwa na asali. Lakini mimi sitakwenda pamoja nanyi, kwa sababu ninyi ni watu wenye shingo ngumu, nisije nikawaangamiza njiani.”
Numbers 16:45“Jitenge mbali na kusanyiko hili ili niweze kuwaangamiza mara moja.” Wakaanguka chini kifudifudi.
Job 34:20Wanakufa ghafula, usiku wa manane; 2 watu wanatikiswa nao hupita; 1 wenye nguvu huondolewa 2 bila mkono wa mwanadamu. 1
Psalms 139:23Ee Mungu, nichunguze, uujue moyo wangu, 2 nijaribu na ujue mawazo yangu. 1
Isaiah 48:4Kwa kuwa nalijua jinsi ulivyokuwa mkaidi; 2 mishipa ya shingo yako ilikuwa chuma, 2 kipaji chako cha uso kilikuwa shaba. 1