Kutoka 38:24
Jumla ya dhahabu iliyopatikana kutokana na sadaka ya kuinuliwa kwa ajili ya kazi ya mahali patakatifu ilikuwa na uzito wa talanta 29 na shekeli 730, + 38:24 Talanta 29 na shekeli 730 ni sawa na tani moja. kulingana na shekeli ya mahali patakatifu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 29:24Viweke vitu hivi vyote mikononi mwa Aroni na wanawe na uviinue mbele za Bwana kuwa sadaka ya kuinuliwa.
Exodus 30:24shekeli 500 za aina nyingine ya mdalasini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, pia hini + 30:24 Hini moja ni sawa na lita 4. ya mafuta ya zeituni.
Leviticus 5:15“Mtu anapokiuka na kutenda dhambi pasipo kukusudia kuhusu mojawapo ya mambo matakatifu ya Bwana, huyo mtu ataleta kwa Bwana kama adhabu kondoo dume mmoja kutoka kundi lake, asiye na dosari na mwenye thamani halisi kifedha, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu. Hii ni sadaka ya hatia.
Leviticus 27:25Kila thamani lazima iwekwe kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, + 27:25 Shekeli moja ya mahali patakatifu ni sawa na gramu 11. gera ishirini kwa shekeli.
Numbers 18:16Watakapokuwa na umri wa mwezi mmoja, ni lazima mtawakomboa kwa bei ya ukombozi iliyowekwa, kwa shekeli tano + 18:16 Shekeli tano za fedha ni sawa na gramu 55. za fedha, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, yenye uzito wa gera ishirini. + 18:16 Gera 20 ni sawa na gramu 55.
1 Chronicles 29:2Kwa uwezo wangu wote nimetenga mali kwa ajili ya Hekalu la Mungu wangu: dhahabu kwa kazi za dhahabu, fedha kwa ajili ya fedha, shaba kwa kazi za shaba, chuma kwa kazi za chuma na miti kwa kazi za miti, vivyo hivyo vito vya shohamu kwa ajili ya kutia kwenye vijalizo, almasi, mawe ya rangi mbalimbali, aina zote za vito vya thamani na marmar; yote haya kwa wingi mno.