Ezekieli 13:14
Nitaubomoa ukuta mlioupaka chokaa na kuuangusha chini ili msingi wake uachwe wazi. Utakapoanguka, mtaangamizwa ndani yake, nanyi mtajua kuwa Mimi ndimi Bwana.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Psalms 11:3Wakati misingi imeharibiwa, 2 mwenye haki anaweza kufanya nini?” 1
Isaiah 28:17Nitaifanya haki kuwa kamba ya kupimia 2 na uadilifu kuwa timazi; 1 mvua ya mawe itafagia kimbilio lenu, huo uongo, 2 nayo maji yatafurikia mahali penu pa kujificha. 1
Jeremiah 6:15Je, wanaona aibu kwa ajili ya tabia yao 2 inayochukiza mno? 1 Hapana, hawana aibu hata kidogo; 2 hawajui hata kuona haya. 1 Kwa hiyo wataanguka miongoni mwa hao walioanguka, 2 watashushwa chini nitakapowaadhibu,” 4 asema Bwana.
Jeremiah 14:15Kwa hiyo, hili ndilo Bwana asemalo kuhusu manabii wanaotabiri kwa jina langu: Mimi sikuwatuma, lakini wanasema, ‘Hakuna upanga wala njaa itakayoigusa nchi hii.’ Manabii hao hao watakufa kwa upanga na njaa.
Ezekiel 13:9Mkono wangu utakuwa dhidi ya manabii ambao huona maono ya uongo na kusema ubashiri wa udanganyifu. Hawatakuwa katika baraza la watu wangu au kuandikwa katika kumbukumbu ya nyumba ya Israeli wala hawataingia katika nchi ya Israeli. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Bwana Mwenyezi.
Ezekiel 13:23kwa hiyo hamtaona tena maono ya uongo wala kufanya ubashiri. Nitawaokoa watu wangu kutoka mikononi mwenu. Nanyi ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana.’ ”