Ezekieli 13:6
Maono yao ni ya uongo na ubashiri wao ni wa udanganyifu. Wao husema, “ Bwana amesema,” wakati Bwana hakuwatuma, bado wakitarajia maneno yao kutimizwa.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
1 Kings 22:6Kwa hiyo mfalme wa Israeli akawaleta pamoja manabii wanaume wapatao mia nne, akawauliza, “Je, niende vitani dhidi ya Ramoth-Gileadi, au niache?” Wakajibu, “Naam, nenda, kwa kuwa Bwana ataiweka Ramoth-Gileadi mkononi mwa mfalme.”
1 Kings 22:15Alipofika, mfalme akamuuliza, “Mikaya, je, twende vitani dhidi ya Ramoth-Gileadi au niache?” Akamjibu, “Shambulia na ushinde, kwa kuwa Bwana atawatia mkononi mwa mfalme.”
1 Kings 22:37Basi mfalme akafa na akaletwa Samaria, nao wakamzika huko.
Jeremiah 5:31Manabii wanatabiri uongo, 2 makuhani wanatawala kwa mamlaka yao wenyewe, 1 nao watu wangu wanapenda hivyo. 2 Lakini mtafanya nini mwisho wake?
Jeremiah 23:31“Naam, mimi niko kinyume na manabii wanaotikisa ndimi zao wenyewe na kusema, ‘ Bwana asema.’
Jeremiah 28:2“Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli asemalo: ‘Nitaivunja nira ya mfalme wa Babeli.