Ezekieli 16:13
Kwa hiyo ulipambwa kwa dhahabu na fedha, nguo zako zilikuwa za kitani safi, hariri na nguo iliyokuwa imetariziwa. Chakula chako kilikuwa unga laini, asali na mafuta ya zeituni. Ukawa mzuri sana ukainuka kuwa malkia.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
12nikaweka hazama puani mwako, vipuli masikioni mwako na taji nzuri sana kichwani mwako.
Cross References
Genesis 17:6Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, kwako yatatoka mataifa nao wafalme watatoka kwako.
Deuteronomy 32:13Akamfanya apande sehemu zilizoinuka za nchi, 2 akamlisha kwa mavuno ya mashamba. 1 Akamlea kwa asali toka mwambani, 2 na kwa mafuta kutoka mwamba mgumu, 1
1 Samuel 12:12“Lakini mlipomwona yule Nahashi mfalme wa Waamoni anakuja dhidi yenu, mliniambia, ‘Hapana, tunataka mfalme atutawale,’ hata ingawa Bwana Mungu wenu alikuwa mfalme wenu.
1 Kings 4:21Mfalme Solomoni akatawala katika falme zote kuanzia Mto Frati hadi nchi ya Wafilisti, hadi kwenye mpaka wa Misri. Nchi hizi zilileta ushuru na zilikuwa chini ya Solomoni, siku zote za maisha yake.
Ezra 5:11Hili ndilo jibu walilotupa: “Sisi ni watumishi wa Mungu wa mbingu na nchi, nasi tunalijenga upya Hekalu ambalo lilijengwa miaka mingi iliyopita, lile ambalo mfalme mkuu wa Israeli alilijenga na kulikamilisha.
Psalms 45:13Utukufu wote una binti mfalme katika chumba chake; 2 vazi lake limefumwa kwa nyuzi za dhahabu. 1