Ezekieli 20:39
“ ‘Kwa habari zenu ninyi, ee nyumba ya Israeli, hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nendeni mkatumikie sanamu zenu, kila mmoja wenu! Lakini baadaye hakika mtanisikiliza mimi nanyi hamtalinajisi tena Jina langu takatifu, kwa matoleo yenu na sanamu zenu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Joshua 24:15Lakini msipoona vyema kumtumikia Bwana, chagueni hivi leo mtakayemtumikia, kama ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ngʼambo Frati, au miungu ya Waamori, ambao mnakaa katika nchi yao. Lakini mimi na nyumba yangu, tutamtumikia Bwana.”
2 Kings 3:13Elisha akamwambia mfalme wa Israeli, “Nina nini mimi nawe? Nenda kwa manabii wa baba yako na manabii wa mama yako.” Mfalme wa Israeli akajibu, “La hasha, kwa sababu ni Bwana ambaye ametuita pamoja sisi wafalme watatu ili atutie mikononi mwa Moabu.”
Proverbs 21:27Dhabihu ya mtu mwovu ni chukizo, 2 si zaidi sana itolewapo kwa nia mbaya! 1
Isaiah 66:3Lakini yeyote atoaye dhabihu ya fahali 2 ni kama yeye auaye mtu, 1 na yeyote atoaye sadaka ya mwana-kondoo, 2 ni kama yule avunjaye shingo ya mbwa. 1 Yeyote atoaye sadaka ya nafaka, 2 ni kama yule aletaye damu ya nguruwe, 1 na yeyote afukizaye uvumba wa kumbukumbu, 2 ni kama yule aabuduye sanamu. 1 Wamejichagulia njia zao wenyewe, 2 nazo nafsi zao zinafurahia machukizo yao. 1
Jeremiah 44:25Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: Ninyi na wake zenu mmeonyesha kwa matendo yenu kile mlichoahidi mliposema, ‘Hakika tutatimiza nadhiri tulizoziweka za kumfukizia uvumba na kummiminia sadaka za kinywaji Malkia wa Mbinguni.’ “Endeleeni basi, fanyeni yale mliyoahidi! Timizeni nadhiri zenu!
Ezekiel 23:37kwa kuwa wamefanya uzinzi na damu imo mikononi mwao. Wamefanya uzinzi na sanamu zao, hata wamewatoa watoto wao walionizalia kuwa kafara, kuwa chakula kwao.