Isaya 66:3
Lakini yeyote atoaye dhabihu ya fahali 2 ni kama yeye auaye mtu, 1 na yeyote atoaye sadaka ya mwana-kondoo, 2 ni kama yule avunjaye shingo ya mbwa. 1 Yeyote atoaye sadaka ya nafaka, 2 ni kama yule aletaye damu ya nguruwe, 1 na yeyote afukizaye uvumba wa kumbukumbu, 2 ni kama yule aabuduye sanamu. 1 Wamejichagulia njia zao wenyewe, 2 nazo nafsi zao zinafurahia machukizo yao. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Leviticus 2:2naye atapeleka kwa makuhani wana wa Aroni. Kuhani atachukua konzi moja iliyojaa unga laini na mafuta pamoja na uvumba wote, na kuuteketeza kama sehemu ya kumbukumbu juu ya madhabahu, sadaka iliyotolewa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza Bwana.
Deuteronomy 23:18Kamwe usilete mapato ya ukahaba ikiwa ni ya mwanamke au ni ya mwanaume katika nyumba ya Bwana Mungu wako kwa ajili ya nadhiri yoyote, kwa sababu Bwana Mungu wako anachukizwa na yote mawili.
Judges 10:14Nendeni mkaililie ile miungu mlioichagua. Hiyo miungu na iwaokoe mnapokuwa katika taabu!”
Proverbs 15:8Bwana huchukia sana dhabihu za waovu, 2 bali maombi ya wanyofu humfurahisha Mungu. 1
Isaiah 1:11Bwana anasema, “Wingi wa sadaka zenu, 2 ni kitu gani kwangu? 1 Ninazo sadaka za kuteketezwa nyingi kupita kiasi, 2 za kondoo dume na mafuta ya wanyama walionona. 1 Sipendezwi na damu za mafahali 2 wala za wana-kondoo na mbuzi. 1
Isaiah 53:6Sisi sote, kama kondoo, tumepotea, 2 kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe, 1 naye Bwana aliweka juu yake 2 maovu yetu sisi sote. 1