Ezekieli 39:17
“Mwanadamu, hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ita kila aina ya ndege na wanyama wote wa mwituni, waambie: ‘Kusanyikeni mje pamoja kutoka pande zote kwa ajili ya dhabihu ninayowaandalia, dhabihu kuu katika milima ya Israeli. Huko mtakula nyama na kunywa damu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 31:54Yakobo akatoa dhabihu juu ya kilima na akawaalika jamaa zake kula chakula. Baada ya kula, wakalala huko.
1 Samuel 16:3Mwalike Yese aje kwenye dhabihu, nami nitakuonyesha utakalofanya. Utamtia mafuta kwa ajili yangu yule nitakayekuonyesha.”
Isaiah 18:6Yote yataachwa kwa ajili ya ndege wawindao wa mlimani 2 na wanyama pori, 1 ndege watajilisha juu yake wakati wote wa kiangazi, 2 nao wanyama pori wakati wote wa masika.
Isaiah 34:6Upanga wa Bwana umeoga katika damu, 2 umefunikwa na mafuta ya nyama: 1 damu ya kondoo na mbuzi, 2 mafuta kutoka figo za kondoo dume. 1 Kwa maana Bwana ana dhabihu huko Bosra, 2 na machinjo makuu huko Edomu. 1
Jeremiah 12:9Je, urithi wangu haukuwa 2 kama ndege wa mawindo wa madoadoa 1 ambaye ndege wengine wawindao 2 humzunguka na kumshambulia? 1 Nenda ukawakusanye pamoja wanyama wote wa mwituni; 2 walete ili wale. 1
Ezekiel 29:5Nitakutupa jangwani, 2 wewe pamoja na samaki wote wa vijito vyako. 1 Utaanguka uwanjani, 2 nawe hutakusanywa au kuchukuliwa. 1 Nitakutoa uwe chakula 2 kwa wanyama wa nchi 2 na ndege wa angani.