Genesis 11:4
Ndipo wakasema, “Njooni, tujijengee mji wenye mnara ambao utafika hadi mbinguni, ili tujipatie jina tusije tukatawanyika usoni pa dunia yote.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
5Lakini Bwana akashuka ili auone mji na mnara ambao wanadamu waliokuwa wanaujenga.
Cross References
Genesis 6:4Wanefili walikuwako duniani siku hizo, na baadaye, hao wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu na kuzaa nao. Wanefili walikuwa mashujaa na watu waliojulikana wa zamani hizo.
Deuteronomy 1:28Twende wapi? Ndugu zetu wametufanya kufa moyo. Wanasema, ‘Watu wa huko wana nguvu zaidi na ni warefu kuliko sisi tulivyo; miji ni mikubwa, yenye kuta zilizofika juu angani. Zaidi ya hayo, tumewaona Waanaki huko.’ ”
Deuteronomy 9:1Sikiliza, ee Israeli. Sasa mnakaribia kuvuka Yordani mwingie na kuwafukuza mataifa makubwa na yenye nguvu kuliko ninyi pamoja na miji mikubwa yenye kuta zilizofika juu angani.
Psalms 49:11Makaburi yao yatabaki kuwa nyumba zao za milele, 2 makao yao vizazi vyote; 1 ingawa walikuwa na mashamba 2 na kuyaita kwa majina yao. 1
Proverbs 10:7Kumbukumbu ya mwenye haki itakuwa baraka, 2 lakini jina la mwovu litaoza. 1
Daniel 4:22Ee mfalme, wewe ndiwe ule mti! Umekuwa mkubwa na mwenye nguvu, nao ukuu wako umekua mpaka kufika juu angani, nayo mamlaka yako yameenea mpaka miisho ya dunia.