Genesis 11:3
Wakasemezana wao kwa wao, “Njooni, tufyatue matofali na tuyachome vizuri kwa moto.” Walitumia matofali badala ya mawe, na lami kwa ajili ya kushikamanishia hayo matofali.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 11:7Njooni, tushuke tuvuruge lugha yao ili wasielewane wao kwa wao.”
Exodus 1:14Wakafanya maisha ya Waisraeli kuwa machungu kwa kufanya kazi ngumu ya kutengeneza lami na kufyatua matofali, na kazi zote za mashambani; katika kazi zao zote ngumu, Wamisri waliwatumia Waisraeli kwa ukatili.
Exodus 5:7“Tangu sasa msiwape hawa watu nyasi za kutengenezea matofali. Wao wakusanye nyasi zao wenyewe.
Psalms 64:5Kila mmoja humtia moyo mwenzake 2 katika mipango mibaya; 1 huzungumza juu ya kuficha mitego yao, 2 nao husema, “Ni nani ataiona?” 1
Ecclesiastes 2:1Nikafikiri moyoni mwangu, “Haya basi, nitakujaribu kwa anasa nione ni lipi lililo jema.” Lakini hilo nalo likaonekana ni ubatili.
Isaiah 9:10“Matofali yameanguka chini, 2 lakini tutajenga tena kwa mawe yaliyochongwa, 1 mitini imeangushwa, 2 lakini tutapanda mierezi badala yake.” 1