Genesis 2:9
Bwana Mungu akafanya aina zote za miti ziote kutoka ardhini, miti yenye kupendeza macho na mizuri kwa chakula. Katikati ya bustani ulikuwepo mti wa uzima na mti wa kujua mema na mabaya.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
10Mto wa kunyeshea bustani ulitiririka toka Edeni, kuanzia hapa ukagawanyika kuwa mito minne.
Cross References
Genesis 3:3lakini Mungu alisema, ‘Kamwe msile tunda la mti ulio katikati ya bustani, wala kuugusa, la sivyo mtakufa.’ ”
Genesis 3:22Kisha Bwana Mungu akasema, “Sasa mtu huyu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya. Sharti asiruhusiwe kunyoosha mkono wake na kuchuma pia kutoka mti wa uzima akala, naye akaishi milele.”
Proverbs 3:18Yeye ni mti wa uzima kwa wale wanaomkumbatia; 2 wale wamshikao watabarikiwa. 1
Isaiah 44:25“mimi huzipinga ishara za manabii wa uongo, 2 na kuwatia upumbavu waaguzi, 1 niyapinduaye maarifa ya wenye hekima, 2 na kuyafanya kuwa upuzi, 1
Ezekiel 31:8Mierezi katika bustani ya Mungu 2 haikuweza kushindana nao, 1 wala misunobari haikuweza 2 kulingana na vitawi vyake, 1 wala miaramoni 2 haikulinganishwa na matawi yake, 1 wala hakukuwa na mti katika bustani ya Mungu 2 wa kulinganisha na uzuri wake. 1
Ezekiel 31:18“ ‘Ni miti ipi ya Edeni inayoweza kulinganishwa nawe kwa fahari na utukufu? Hata hivyo, wewe pia, utashushwa chini pamoja na miti ya Edeni mpaka kuzimu, utalala miongoni mwa wasiotahiriwa, pamoja na wale waliouawa kwa upanga. “ ‘Huyu ni Farao pamoja na makundi yake yote ya wajeuri, asema Bwana Mwenyezi.’ ”