Genesis 26:18
Ndipo Isaki akavichimbua tena vile visima vya maji ambavyo vilichimbwa siku zile za Abrahamu baba yake, ambavyo Wafilisti walivifukia baada ya kufa Abrahamu, akavipa majina yale yale ambayo baba yake alikuwa amevipa.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
17Basi Isaki akatoka huko akajenga kambi katika Bonde la Gerari, akaishi huko.
19Watumishi wa Isaki wakachimba katika lile bonde wakagundua huko kisima chenye maji safi.
Cross References
Genesis 21:31Hivyo mahali pale pakaitwa Beer-Sheba, kwa sababu watu wawili waliapiana hapo.
Psalms 16:4Huzuni itaongezeka kwa wale 2 wanaokimbilia miungu mingine. 1 Sitazimimina sadaka zao za damu 2 au kutaja majina yao midomoni mwangu. 1
Zechariah 13:2“Katika siku hiyo, nitayakatilia mbali majina ya sanamu kutoka nchi, nayo hayatakumbukwa tena,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote. “Nitaondoa manabii wao pamoja na roho ya uchafu katika nchi.