Genesis 3:14
Hivyo Bwana Mungu akamwambia nyoka, “Kwa kuwa umefanya hili, 1 “Umelaaniwa kuliko wanyama wote 2 wa kufugwa na wa porini! 1 Utatambaa kwa tumbo lako 2 na kula mavumbi 2 siku zote za maisha yako. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 3:1Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa porini ambao Bwana Mungu aliwafanya. Nyoka akamwambia mwanamke, “Ati kweli Mungu alisema, ‘Kamwe msile matunda ya mti wowote wa bustanini’?”
Exodus 21:28“Kama fahali akimuua mwanaume au mwanamke kwa kumpiga kwa pembe, fahali huyo ni lazima auawe kwa kupigwa mawe, na nyama yake haitaliwa. Lakini mwenye fahali huyo hatawajibika.
Deuteronomy 28:15Hata hivyo, kama hutamtii Bwana Mungu wako na kuzishika kwa bidii amri zake zote na maagizo ninayokupa leo, laana hizi zote zitakuja juu yako na kukupata:
Isaiah 29:4Utakaposhushwa, utanena kutoka ardhini, 2 utamumunya maneno yako kutoka mavumbini. 1 Sauti yako itatoka katika nchi kama vile ya mzimu, 2 utanongʼona maneno yako toka mavumbini. 1
Micah 7:17Wataramba mavumbi kama nyoka, 2 kama viumbe vitambaavyo juu ya ardhi. 1 Watatoka nje ya mapango yao wakitetemeka; 2 watamgeukia Bwana Mungu wetu kwa hofu 2 nao watakuogopa. 1