Genesis 34:5
Yakobo aliposikia kwamba binti yake Dina amenajisiwa, wanawe walikuwa mashambani wakichunga mifugo yake, kwa hiyo akalinyamazia jambo hilo mpaka waliporudi nyumbani.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
4Shekemu akamwambia baba yake Hamori, “Nipatie msichana huyu awe mke wangu.”
6Kisha Hamori baba yake Shekemu akaenda kuzungumza na Yakobo.
Cross References
Genesis 37:13naye Israeli akamwambia Yosefu, “Kama ujuavyo, ndugu zako wanachunga makundi huko karibu na Shekemu. Njoo, nitakutuma kwao.” Yosefu akajibu, “Vema sana, niko tayari.”
Leviticus 10:3Kisha Mose akamwambia Aroni, “Hili ndilo alilonena Bwana wakati aliposema: 1 “ ‘Miongoni mwa wale watakaonikaribia 2 nitajionyesha kuwa mtakatifu; 1 machoni pa watu wote 2 nitaheshimiwa.’ ” Aroni akanyamaza.
1 Samuel 16:11Hivyo akamuuliza Yese, “Je, hawa ndio wana pekee ulio nao?” Yese akajibu, “Bado yuko mdogo kuliko wote, lakini anachunga kondoo.” Samweli akasema, “Tuma aitwe; hatutaketi mpaka afike.”
2 Samuel 13:22Absalomu hakusema neno lolote na Amnoni, likiwa zuri au baya, kwa kuwa alimchukia Amnoni kwa sababu alikuwa amemtia aibu Tamari, dada yake. 1 Absalomu Amuua Amnoni
Luke 15:25“Wakati huo, yule mwana mkubwa alikuwa shambani. Alipokaribia nyumbani, akasikia sauti ya nyimbo na watu wakicheza.