Genesis 37:8
Ndugu zake wakamwambia, “Wewe unakusudia kututawala? Hivi kweli wewe utatutawala sisi?” Wakaongeza kumchukia zaidi kwa sababu ya ndoto yake pamoja na yale aliyowaambia.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 49:26Baraka za baba yako ni kubwa 2 kuliko baraka za milima ya kale, 2 nyingi kuliko vilima vya kale. 1 Baraka hizo zote na zikae juu ya kichwa cha Yosefu, 2 juu ya paji la yule mkuu miongoni mwa ndugu zake. 1
1 Samuel 10:27Lakini baadhi ya watu wakorofi walisema, “Huyu mtu atawezaje kutuokoa?” Wakamdharau na wala hawakumletea zawadi. Lakini Sauli akanyamaza kimya.
1 Samuel 18:8Sauli akakasirika sana; sehemu hii ya kurudia rudia ya wimbo huu ilimkasirisha sana. Akafikiri kuwa, “Wamempa Daudi makumi elfu, lakini mimi wamenipa elfu tu. Apate nini zaidi isipokuwa ufalme?”
Psalms 118:22Jiwe walilolikataa waashi, 2 limekuwa jiwe kuu la pembeni. 1
Luke 20:17Lakini Yesu akawakazia macho, akasema, “Basi ni nini maana ya yale yaliyoandikwa: 1 “ ‘Jiwe walilolikataa waashi, 2 limekuwa jiwe kuu la pembeni’?
Acts 7:35“Huyu ndiye Mose yule waliyemkataa wakisema, ‘Ni nani aliyekufanya mtawala na mwamuzi juu yetu?’ Alikuwa ametumwa na Mungu mwenyewe kuwa mtawala na mkombozi wao, kwa njia ya yule malaika aliyemtokea katika kile kichaka.