Genesis 38:26
Yuda akavitambua na kusema, “Yeye ana haki kuliko mimi, kwa kuwa sikumkabidhi kwa mwanangu Shela ili awe mkewe.” Tangu hapo hakukutana naye kimwili tena.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
27Wakati ulipofika wa kujifungua, kukawa na wana mapacha tumboni mwake.
Cross References
Genesis 4:1Adamu akakutana kimwili na mkewe Eva, naye akapata mimba, akamzaa Kaini. Eva akasema, “Kwa msaada wa Bwana nimemzaa mwanaume.”
Genesis 38:14alivua mavazi yake ya ujane, akajifunika kwa shela ili asifahamike, akaketi kwenye mlango wa Enaimu, ambao upo njiani kuelekea Timna. Akafanya hivyo kwa sababu aliona kwamba, ingawa Shela amekua, lakini alikuwa hajakabidhiwa kwake kuwa mkewe.
1 Samuel 24:18Sasa umeniambia juu ya mema uliyonitendea. Bwana alinitia mikononi mwako, lakini wewe hukuniua.
2 Samuel 20:3Daudi aliporudi katika jumba lake la kifalme huko Yerusalemu, aliwachukua wale masuria kumi aliokuwa amewaacha ili kuangalia jumba la kifalme na kuwaweka ndani ya nyumba chini ya ulinzi. Akawapa mahitaji yao lakini hakukutana nao kimwili. Waliwekwa kifungoni wakaishi kama wajane mpaka kifo chao.
Job 4:5Lakini sasa hii taabu imekujia wewe, 2 nawe unashuka moyo; 1 imekupiga wewe, 2 nawe unafadhaika. 1
Job 34:32Nifundishe nisichoweza kuona; 2 kama nimekukosea, sitafanya hivyo tena.’ 1