Genesis 42:28
Akawaambia ndugu zake, “Fedha yangu imerudishwa. Iko ndani ya gunia langu.” Mioyo yao ikazimia, na kila mmoja akamgeukia mwenzake wakitetemeka, wakaulizana, “Ni nini hiki Mungu alichotufanyia?”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 42:36Yakobo baba yao akawaambia, “Ninyi mmenipokonya watoto wangu. Yosefu hayupo na Simeoni hayupo tena na sasa mnataka kumchukua Benyamini. Kila kitu ni kinyume nami!”
Leviticus 26:36“ ‘Kwa habari ya wenzenu wale watakaobaki, nitaifanya mioyo yao kuwa na hofu kuu katika nchi za adui zao, kiasi kwamba sauti ya jani linalopeperushwa na upepo itawafanya wakimbie. Watakimbia kana kwamba wanakimbia upanga, nao wataanguka, ingawa hakuna anayewafukuza.
1 Kings 10:5chakula kilichokuwa mezani pake, jinsi maafisa wake walivyokaa, wahudumu katika majoho yao, wanyweshaji wake na sadaka za kuteketezwa alizotoa katika hekalu la Bwana, alipatwa na mshangao.
Song of Solomon 5:6Nilimfungulia mpenzi wangu, 2 lakini mpenzi wangu alishaondoka; 2 alikuwa amekwenda zake. 1 Moyo wangu ulishuka kwa kuondoka kwake. 2 Nilimtafuta lakini sikumpata. 2 Nilimwita lakini hakunijibu. 1
Lamentations 2:17Bwana amefanya lile alilolipanga; 2 ametimiza neno lake 2 aliloliamuru siku za kale. 1 Amekuangusha bila huruma, 2 amewaacha adui wakusimange, 2 ametukuza pembe ya adui yako. 1
Amos 3:6Je, tarumbeta inapopigwa mjini kujulisha hatari, 2 watu hawatetemeki? 1 Mji upatwapo na maafa, 2 je, si Bwana amesababisha? 1