Genesis 42:38
Lakini Yakobo akasema, “Mwanangu hatashuka huko pamoja nanyi; ndugu yake amekufa naye ndiye peke yake aliyebaki. Ikiwa atapatwa na madhara katika safari mnayoiendea, mtashusha kichwa changu chenye mvi kaburini kwa masikitiko.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 30:22Ndipo Mungu akamkumbuka Raheli, akasikia maombi yake na akafungua tumbo lake.
Genesis 37:33Baba yao akalitambua akasema, “Hili ni joho la mwanangu! Mnyama mkali amemrarua. Hakika Yosefu ameraruliwa vipande vipande.”
Genesis 42:4Lakini Yakobo hakumtuma Benyamini, ndugu yake Yosefu, pamoja na wengine, kwa sababu aliogopa asije akapatwa na madhara.
Genesis 43:13Mchukueni ndugu yenu pia mrudi kwa huyo mtu mara moja.
Genesis 44:22Nasi tukamwambia bwana wangu, ‘Kijana hawezi kumwacha baba yake; akimwacha, baba yake atakufa.’
1 Kings 2:6Shughulika naye kwa kadiri ya hekima yako, lakini usiache kichwa chake chenye mvi kishukie kaburi kwa amani.