Genesis 43:34
Wakati walipelekewa sehemu ya chakula kutoka mezani mwa Yosefu, sehemu ya Benyamini ilikuwa mara tano zaidi ya sehemu ya wale wengine. Kwa hiyo wakanywa na kufurahi pamoja naye.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
1 Samuel 1:5Lakini alimpa Hana fungu maradufu kwa sababu alimpenda, ingawa Bwana alikuwa amemfunga tumbo.
2 Samuel 11:8Kisha Daudi akamwambia Uria, “Teremka nyumbani kwako ukanawe miguu yako.” Basi Uria akaondoka kutoka kwenye jumba la kifalme, tena zawadi zikamfuata kutoka kwa mfalme.
Ecclesiastes 9:7Nenda, kula chakula chako kwa furaha, unywe divai yako kwa moyo wa shangwe, kwa maana sasa Mungu anakubali unachofanya.
Song of Solomon 5:1Nimekuja kwenye bustani yangu, dada yangu, 2 bibi arusi wangu; 1 nimekusanya manemane yangu pamoja 2 na kikolezo changu. 1 Nimekula sega langu la asali na asali yangu; 2 nimekunywa divai yangu na maziwa yangu. Marafiki 1 Kuleni, enyi marafiki, mnywe; 1 kunyweni ya kutosha, ee wapenzi. 1 Shairi La Nne Mpendwa 1
Matthew 11:19Mwana wa Adamu alikuja akila na kunywa, nao wanasema, ‘Tazameni huyu mlafi na mlevi, rafiki wa watoza ushuru na “wenye dhambi.” ’ Lakini hekima huthibitishwa kuwa kweli kwa matendo yake.” 1 Onyo Kwa Miji Isiyotubu (Luka 10:13-15)