Genesis 48:5
“Sasa basi, wanao wawili waliozaliwa kwako huku Misri kabla sijaja hapa kwako watahesabiwa kuwa ni wangu; Efraimu na Manase watakuwa wangu, kama vile Reubeni na Simeoni walivyo wangu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 41:51Yosefu akamwita mzaliwa wake wa kwanza Manase, akisema, “Ni kwa sababu Mungu amenifanya nisahau taabu zangu zote pamoja na jamaa yote ya nyumba ya baba yangu.”
Genesis 46:20Huko Misri, Asenathi binti wa Potifera, aliyekuwa kuhani wa mji wa Oni, + 46:20 Yaani Heliopoli (Mji wa Jua). alimzalia Yosefu wana wawili, Manase na Efraimu. 1
Numbers 1:10kutoka wana wa Yosefu: 2 kutoka Efraimu, ni Elishama mwana wa Amihudi; 2 kutoka Manase, ni Gamalieli mwana wa Pedasuri; 1
Numbers 26:28Wazao wa Yosefu kwa koo zao kutoka kwa Manase na kwa Efraimu walikuwa:
Joshua 14:4kwa kuwa wana wa Yosefu walikuwa makabila mawili; Manase na Efraimu. Walawi hawakupata mgawo wa ardhi, bali walipewa miji tu kwa ajili ya kuishi, pamoja na maeneo ya malisho kwa ajili ya makundi yao ya kondoo, mbuzi na ngʼombe wao.
1 Chronicles 5:1Wana wa Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Israeli (yeye alikuwa mzaliwa wa kwanza, lakini kwa kuwa alikinajisi kitanda cha baba yake, haki zake za mzaliwa wa kwanza walipewa wana wa Yosefu mwana wa Israeli. Hivyo hakuorodheshwa kwenye orodha ya ukoo wao kulingana na haki yake ya kuzaliwa.