Hebrews 2:14
Basi kwa kuwa watoto wana nyama na damu, yeye pia alishiriki katika ubinadamu wao, ili kwa kifo chake, apate kumwangamiza huyo mwenye nguvu za mauti, yaani ibilisi,
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
15na kuwaweka huru wale waliokuwa utumwani maisha yao yote kwa sababu ya kuogopa mauti.
Cross References
Isaiah 7:14Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara: Bikira atachukua mimba, naye atamzaa mwana, na ataitwa Imanueli. + 7:14 Imanueli maana yake Mungu yu pamoja nasi.
Isaiah 53:12Kwa hiyo nitamgawia sehemu miongoni mwa wakuu, 2 naye atagawana nyara pamoja na wenye nguvu, 1 kwa sababu aliyamimina maisha yake hadi mauti, 2 naye alihesabiwa pamoja na wakosaji. 1 Kwa kuwa alichukua dhambi za wengi, 2 na kuwaombea wakosaji.
Matthew 25:41“Kisha atawaambia wale walio upande wake wa kushoto, ‘Ondokeni kwangu, ninyi mliolaaniwa, nendeni kwenye moto wa milele ulioandaliwa kwa ajili ya ibilisi na malaika zake.
John 12:24Amin, amin nawaambia, mbegu ya ngano isipoanguka ardhini na kufa, hubakia kama mbegu peke yake. Lakini ikifa huzaa mbegu nyingi.
Romans 8:3Kwa maana kile ambacho sheria haikuwa na uwezo wa kufanya, kwa vile ilivyokuwa dhaifu katika mwili, Mungu kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe kwa mfano wa mwanadamu mwenye mwili ulio wa dhambi na kwa ajili ya dhambi, yeye aliihukumu dhambi katika mwili,
1 Corinthians 15:50Ndugu zangu nisemalo ni hili: nyama na damu haviwezi kuurithi ufalme wa Mungu, wala kuharibika kurithi kutokuharibika.