Hebrews 7:18
Kwa upande mmoja, ile amri ya mwanzo isiyofaa na dhaifu imebatilishwa
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
17Kwa maana imeshuhudiwa kwamba: 1 “Wewe ni kuhani milele, 2 kwa mfano wa Melkizedeki.”
Cross References
Acts 13:39Kwa kupitia yeye, kila mtu amwaminiye anahesabiwa haki kwa kila kitu ambacho asingeweza kuhesabiwa haki kwa sheria ya Mose.
Romans 8:3Kwa maana kile ambacho sheria haikuwa na uwezo wa kufanya, kwa vile ilivyokuwa dhaifu katika mwili, Mungu kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe kwa mfano wa mwanadamu mwenye mwili ulio wa dhambi na kwa ajili ya dhambi, yeye aliihukumu dhambi katika mwili,
Galatians 3:17Ninachotaka kusema ni kwamba, sheria, ambayo ilitolewa miaka 430 baadaye, haitangui Agano lililothibitishwa na Mungu ili kuibatilisha ahadi ile.
Galatians 4:21Niambieni, ninyi mnaotaka kuwa chini ya sheria, je, hamjui sheria inavyosema?
Hebrews 7:11Kama ukamilifu ungeweza kupatikana kwa njia ya ukuhani wa Walawi (kwa kuwa katika msingi huo, sheria ilitolewa kwa watu), kwa nini basi imekuwepo haja ya kuja kuhani mwingine: kuhani kwa mfano wa Melkizedeki, wala si kwa mfano wa Aroni?
Hebrews 8:7Kwa maana kama hapakuwa na kasoro katika lile agano la kwanza, pasingekuwa na haja ya kutafuta nafasi kwa ajili ya jingine.