Hosea 10:1
Israeli alikuwa mzabibu uliostawi sana, 2 alijizalia matunda mwenyewe. 1 Kadiri matunda yake yalivyoongezeka, 2 alijenga madhabahu zaidi; 1 kadiri nchi yake ilivyostawi, 2 alipamba mawe yake ya ibada. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
1 Kings 14:23Pia wakajijengea mahali pa juu pa kuabudia miungu, mawe ya kuabudiwa na nguzo za Ashera juu ya kila kilima kilichoinuka na kila mti uliotanda.
Isaiah 5:4Ni nini zaidi ambacho kingeweza kufanyika kwa shamba langu la mizabibu 2 kuliko yale niliyofanya? 1 Nilipotazamia kupata zabibu nzuri, 2 kwa nini lilizaa zabibu mbaya tu? 1
Jeremiah 2:28Iko wapi basi ile miungu mliyojitengenezea? 2 Yenyewe na ije kama inaweza kuwaokoa 2 wakati mko katika taabu! 1 Kwa maana mna miungu mingi 2 kama mlivyo na miji, ee Yuda. 1
Jeremiah 11:17Bwana Mwenye Nguvu Zote, aliyekupanda, ametamka maafa kwa ajili yako, kwa sababu nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda mmefanya maovu na kunikasirisha kwa kumfukizia Baali uvumba. 1 Shauri Baya Dhidi Ya Yeremia
Hosea 2:8Gomeri hajakubali kuwa mimi ndiye 2 niliyempa nafaka, divai mpya na mafuta, 1 niliyemwongezea fedha na dhahabu waliyoitumia 2 kwa kumtumikia Baali. 1
Hosea 8:4Wanaweka wafalme bila idhini yangu, 2 wamechagua wakuu bila kibali changu. 1 Kwa fedha zao na dhahabu 2 wamejitengenezea sanamu kwa ajili 2 ya maangamizi yao wenyewe. 1