Hosea 2:7
Gomeri atawafuatia wapenzi wake lakini hatawapata; 2 atawatafuta lakini hatawapata. 1 Kisha atasema, 2 ‘Nitarudi kwa mume wangu kama kwanza, 1 kwa maana nilikuwa na hali njema zaidi 2 kuliko sasa.’ 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Deuteronomy 8:17Mnaweza kusema, “Uwezo wangu na nguvu za mikono yangu ndizo zilizonipatia utajiri huu.”
2 Chronicles 28:20Hivyo Tiglath-Pileseri mfalme wa Ashuru akaja kumtesa badala ya kumsaidia.
Nehemiah 9:25Wakateka miji yenye ngome na nchi yenye rutuba, wakamiliki nyumba zilizojazwa na vitu vizuri vya kila aina, visima vilivyochimbwa tayari, mashamba ya mizabibu, mashamba ya mizeituni na miti yenye matunda kwa wingi. Wakala, wakashiba nao wakanawiri sana, wakajifurahisha katika wema wako mwingi.
Isaiah 30:2wale washukao kwenda Misri 2 bila kutaka shauri langu, 1 wanaotafuta msaada wa ulinzi wa Farao, 2 watafutao kivuli cha Misri kwa ajili ya kimbilio. 1
Isaiah 31:1Ole wao wale washukao Misri kwa ajili ya msaada, 2 wale wategemeao farasi, 1 wanaoweka tumaini katika wingi wa magari yao ya vita, 2 na katika nguvu nyingi za wapanda farasi, 1 lakini hawamwangalii yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, 2 wala hawatafuti msaada kwa Bwana. 1
Jeremiah 2:28Iko wapi basi ile miungu mliyojitengenezea? 2 Yenyewe na ije kama inaweza kuwaokoa 2 wakati mko katika taabu! 1 Kwa maana mna miungu mingi 2 kama mlivyo na miji, ee Yuda. 1