Isaiah 1:29
“Mtaaibika kwa sababu ya hiyo mialoni 2 ambayo mlifurahia, 1 mtafadhaika kwa sababu ya bustani 2 mlizozichagua. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
28Lakini waasi na wenye dhambi wote wataangamizwa, 2 nao wanaomwacha Bwana wataangamia. 1
30Mtakuwa kama mwaloni wenye majani yanayonyauka, 2 kama bustani isiyokuwa na maji. 1
Cross References
Isaiah 31:7Kwa kuwa katika siku ile kila mmoja wenu atazikataa sanamu za fedha na za dhahabu zilizotengenezwa kwa mikono yenu yenye dhambi. 1
Isaiah 57:5Mnawaka tamaa katikati ya mialoni 2 na chini ya kila mti uliotanda matawi; 1 mnawatoa kafara watoto wenu kwenye mabonde 2 na chini ya majabali yenye mianya. 1
Isaiah 66:17“Watu wote wanaojiweka wakfu na kujitakasa wenyewe ili kwenda bustanini, wakimfuata aliye katikati ya wale ambao hula nyama za nguruwe na panya pamoja na vitu vingine vilivyo machukizo, watafikia mwisho wao pamoja,” asema Bwana.
Jeremiah 3:6Wakati wa utawala wa Mfalme Yosia, Bwana aliniambia, “Umeona kile Israeli asiye mwaminifu amekifanya? Amepanda juu ya kila kilima kirefu, na chini ya kila mti uliotanda na amefanya uzinzi huko.
Ezekiel 16:63Basi, nitakapofanya upatanisho kwa ajili yako, kwa yale yote uliyoyatenda, utakumbuka na kuaibika, nawe kamwe hutafumbua tena kinywa chako kwa sababu ya aibu yako, asema Bwana Mwenyezi.’ ”
Hosea 4:13Wanatoa dhabihu juu ya vilele vya milima 2 na sadaka za kuteketezwa juu ya vilima, 1 chini ya mialoni, milibua na miela, 2 ambako kuna vivuli vizuri. 1 Kwa hiyo binti zenu wamegeukia ukahaba 2 na wake za wana wenu uzinzi. 1