Isaiah 18:7
Wakati huo matoleo yataletwa kwa Bwana Mwenye Nguvu Zote 1 kutoka kwa taifa la watu warefu wenye ngozi nyororo, 2 kutoka kwa taifa linaloogopwa mbali na karibu, 1 kutoka taifa gomvi lenye lugha ngeni, 2 ambalo nchi yao imegawanywa kwa mito, matoleo yataletwa katika Mlima Sayuni, mahali pa Jina la Bwana Mwenye Nguvu Zote.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Psalms 68:29Kwa sababu ya Hekalu lako Yerusalemu 2 wafalme watakuletea zawadi. 1
Psalms 72:9Makabila ya jangwani watamsujudia, 2 na adui zake wataramba mavumbi. 1
Isaiah 18:4Hili ndilo Bwana aliloniambia: 2 “Nitatulia kimya na kutazama 2 kutoka maskani yangu, 1 kama joto linalometameta katika mwanga wa jua, 2 kama wingu la umande 2 katika joto la wakati wa mavuno.” 1
Isaiah 45:14Hili ndilo asemalo Bwana: 1 “Mazao ya Misri na bidhaa za Kushi, 2 nao wale Waseba warefu, 1 watakujia na kuwa wako, 2 watakujia wakijikokota nyuma yako, 2 watakujia wamefungwa minyororo. 1 Watasujudu mbele yako 2 wakikusihi na kusema, 1 ‘Hakika Mungu yu pamoja nawe, 2 wala hakuna mwingine; 2 hakuna Mungu mwingine.’ ” 1
Micah 4:13“Inuka upure, ee Binti Sayuni, 2 kwa kuwa nitakupa pembe za chuma; 1 nitakupa kwato za shaba 2 na utavunja vipande vipande mataifa mengi.” 1 Utatoa mapato yao waliopata kwa udanganyifu kwa Bwana, 2 utajiri wao kwa Bwana wa dunia yote.
Zechariah 14:16Kisha walionusurika katika mataifa yote ambayo yaliushambulia Yerusalemu watakuwa wakipanda Yerusalemu kila mwaka kumwabudu Mfalme, Bwana Mwenye Nguvu Zote na kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda.