Isaiah 45:14
Hili ndilo asemalo Bwana: 1 “Mazao ya Misri na bidhaa za Kushi, 2 nao wale Waseba warefu, 1 watakujia na kuwa wako, 2 watakujia wakijikokota nyuma yako, 2 watakujia wamefungwa minyororo. 1 Watasujudu mbele yako 2 wakikusihi na kusema, 1 ‘Hakika Mungu yu pamoja nawe, 2 wala hakuna mwingine; 2 hakuna Mungu mwingine.’ ” 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
15Hakika wewe u Mungu unayejificha, 2 Ee Mungu na Mwokozi wa Israeli. 1
Cross References
Numbers 13:32Wakaeneza taarifa mbaya miongoni mwa Waisraeli kuhusu nchi waliyoipeleleza. Wakasema, “Nchi tuliyoipeleleza hula watu waishio ndani yake. Watu wote tuliowaona huko ni majitu.
Esther 8:17Katika kila jimbo na katika kila jiji, popote waraka wa mfalme ulipofika, kulikuwepo furaha na shangwe miongoni mwa Wayahudi, pamoja na karamu na kushangilia. Na watu wengi wa mataifa mengine wakajifanya Wayahudi kwa sababu ya kuwahofu Wayahudi.
Psalms 68:30Mkemee mnyama aliyeko kwenye manyasi, 2 kundi la mafahali katikati ya ndama za mataifa. 1 Na walete minara ya madini ya fedha wakinyenyekea. 2 Tawanya mataifa yapendayo vita. 1
Psalms 149:6Sifa za Mungu na ziwe vinywani mwao 2 na upanga ukatao kuwili mikononi mwao, 1
Isaiah 10:33Tazama, Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, 2 atayakata matawi kwa nguvu kuu. 1 Miti mirefu sana itaangushwa, 2 ile mirefu itashushwa chini. 1
Isaiah 18:7Wakati huo matoleo yataletwa kwa Bwana Mwenye Nguvu Zote 1 kutoka kwa taifa la watu warefu wenye ngozi nyororo, 2 kutoka kwa taifa linaloogopwa mbali na karibu, 1 kutoka taifa gomvi lenye lugha ngeni, 2 ambalo nchi yao imegawanywa kwa mito, matoleo yataletwa katika Mlima Sayuni, mahali pa Jina la Bwana Mwenye Nguvu Zote.