Isaiah 19:1
Neno kuhusu Misri: 1 Tazama, Bwana amepanda juu ya wingu liendalo kwa haraka 2 naye anakuja Misri. 1 Sanamu za Misri zinatetemeka mbele yake, 2 nayo mioyo ya Wamisri inayeyuka ndani yao. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 12:12“Usiku huo huo nitapita katika nchi yote ya Misri na kumuua kila mzaliwa wa kwanza, wa wanadamu na wa wanyama, nami nitaihukumu miungu yote ya Misri. Mimi ndimi Bwana.
Numbers 33:4waliokuwa wakizika wazaliwa wao wa kwanza wote, ambao Bwana alikuwa amewaua katikati yao, kwa kuwa Bwana alikuwa ameleta hukumu juu ya miungu yao. 1
Joshua 2:9akawaambia, “Ninajua kuwa Bwana amewapa nchi hii na hofu kuu imetuangukia kwa sababu yenu, kiasi kwamba wote waishio katika nchi hii wanayeyuka kwa hofu kwa sababu yenu.
Joshua 2:24Wakamwambia Yoshua, “Hakika Bwana ametupa nchi yote mikononi mwetu; watu wote wanayeyuka kwa hofu kwa sababu yetu.”
Psalms 18:10Alipanda juu ya kerubi akaruka, 2 akapaa juu kwa mbawa za upepo. 1
Psalms 68:33mwimbieni sifa yeye apandaye mbingu za kale zilizo juu, 2 yeye angurumaye kwa sauti kuu. 1