Isaya 27:11
Wakati vijiti vyake vimekauka, huvunjwa 2 nao wanawake huja na kuwasha navyo moto. 1 Kwa kuwa hili ni taifa lisilo na ufahamu, 2 kwa hiyo yeye aliyewafanya hana huruma juu yao, 2 Muumba wao hawaonyeshi fadhili.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 6:6Bwana akasikitika kwamba alimuumba mwanadamu duniani, moyo wa Mungu ukajaa masikitiko.
Deuteronomy 4:6Zishikeni kwa uangalifu, kwa kuwa hii itaonyesha hekima na ufahamu wenu kwa mataifa, ambayo yatasikia kuhusu amri zote hizi, nao watasema, “Hakika taifa hili kubwa ni watu wenye hekima na ufahamu.”
Deuteronomy 32:28Wao ni taifa lisilo na akili, 2 hakuna busara ndani yao. 1
Psalms 80:15mche ulioupanda kwa mkono wako wa kuume, 1 mwana uliyemlea 2 kwa ajili yako mwenyewe. 1
Isaiah 1:3Ngʼombe anamjua bwana wake, 2 naye punda anajua hori la mmiliki wake, 1 lakini Israeli hajui, 2 watu wangu hawaelewi.” 1
Isaiah 43:1Lakini sasa hili ndilo asemalo Bwana, 2 yeye aliyekuumba, ee Yakobo, 2 yeye aliyekuhuluku, ee Israeli: 1 “Usiogope kwa maana nimekukomboa, 2 nimekuita wewe kwa jina lako, wewe u wangu. 1