Isaya 27:10
Mji ulio na boma umebaki ukiwa, 2 makao yaliyotelekezwa, yaliyoachwa kama jangwa. 1 Huko ndama hulisha, 2 huko hujilaza, 2 wanakwanyua matawi yake. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Isaiah 5:9Bwana Mwenye Nguvu Zote amesema nikisikia: 2 “Hakika nyumba kubwa zitakuwa ukiwa, 2 nayo majumba ya fahari yatabaki bila kukaliwa. 1
Isaiah 7:25Kuhusu vilima vyote vilivyokuwa vikilimwa kwa jembe, hamtakwenda huko tena kwa ajili ya hofu ya michongoma na miiba. Patakuwa mahali ambapo ngʼombe wataachiwa huru, na kondoo kukimbia kimbia.
Isaiah 17:9Katika siku ile miji yao iliyo imara, ambayo waliihama kwa sababu ya Waisraeli, itakuwa kama mahali palipoachwa pa vichaka na magugu. Nayo yote itakuwa ukiwa. 1
Isaiah 25:2Umeufanya mji kuwa lundo la kifusi, 2 mji wenye ngome kuwa magofu, 1 ngome imara ya wageni kuwa si mji tena, 2 wala hautajengwa tena kamwe. 1
Isaiah 64:10Miji yako mitakatifu imekuwa jangwa; 2 hata Sayuni ni jangwa, Yerusalemu ni ukiwa. 1
Jeremiah 26:18“Mika Mmoreshethi alitoa unabii katika siku za Hezekia mfalme wa Yuda. Akawaambia watu wote wa Yuda, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: 1 “ ‘Sayuni italimwa kama shamba, 2 Yerusalemu itakuwa lundo la kokoto, 1 na kilima cha Hekalu kitakuwa kichuguu 2 kilichofunikwa na vichaka.’