Isaiah 41:11
“Wote walioona hasira dhidi yako 2 hakika wataaibika na kutahayarika, 1 wale wakupingao 2 watakuwa kama vile si kitu, na kuangamia. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 12:29Ilipofika usiku wa manane, Bwana akawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika Misri, kuanzia mzaliwa wa kwanza wa Farao, mrithi wa kiti cha ufalme, hadi mzaliwa wa kwanza wa mfungwa, aliyekuwa gerezani, na wazaliwa wa kwanza wa mifugo yote pia.
Isaiah 29:8kama vile mtu aliye na njaa aotavyo kuwa anakula, 2 lakini huamka, bado njaa yake ingalipo, 1 kama vile mtu mwenye kiu aotavyo kuwa anakunywa maji, 2 lakini huamka akiwa anazimia, akiwa bado angali ana kiu. 1 Hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa makundi yote ya mataifa 2 yanayopigana dhidi ya Mlima Sayuni. 1
Isaiah 41:24Lakini ninyi ni zaidi ya bure kabisa, 2 na kazi zenu hazifai kitu kabisa; 2 yeye awachaguaye ni chukizo sana. 1
Isaiah 45:24Watasema kuhusu mimi, 2 ‘Katika Bwana peke yake 2 ndiko kuna haki na nguvu.’ ” 1 Wote ambao wamemkasirikia Mungu 2 watamjia yeye, nao watatahayarika. 1
Isaiah 49:26Nitawafanya wale wanaokuonea kula nyama yao wenyewe, 2 watalewa kwa damu yao wenyewe, 2 kama vile kwa mvinyo. 1 Ndipo wanadamu wote watajua 2 ya kuwa Mimi, Bwana, ni Mwokozi wako, 2 Mkombozi wako, niliye Mwenye Nguvu wa Yakobo.”
Isaiah 54:17Hakuna silaha itakayofanyizwa dhidi yako 2 itakayofanikiwa, 1 nawe utauthibitisha kuwa mwongo 2 kila ulimi utakaokushtaki. 1 Huu ndio urithi wa watumishi wa Bwana 2 na hii ndiyo haki yao itokayo kwangu,” 4 asema Bwana.