Isaya 41:15
“Tazama, nitakufanya chombo cha kupuria, 2 kipya na chenye makali, chenye meno mengi. 1 Utaipura milima na kuiponda 2 na kuvifanya vilima kuwa kama makapi. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Joshua 17:18bali pia nchi hii ya kilima yenye msitu. Ifyekeni, nayo mipaka yake itakuwa yenu umbali mtakaoweza kufika. Ingawa Wakanaani wana magari ya chuma, nao wana nguvu, mwaweza kuwafukuza humo.”
Job 41:30Sehemu zake za chini kwenye tumbo 2 zina menomeno na mapengo kama vigae vya chungu, 1 zikiacha mburuzo kwenye matope 2 kama chombo chenye meno cha kupuria. 1
Isaiah 21:10Ee watu wangu, mliopondwa kwenye sakafu ya kupuria, 2 ninawaambia kile nilichokisikia 1 kutoka kwa Bwana Mwenye Nguvu Zote, 2 kutoka kwa Mungu wa Israeli. 1 Unabii Dhidi Ya Edomu
Micah 4:13“Inuka upure, ee Binti Sayuni, 2 kwa kuwa nitakupa pembe za chuma; 1 nitakupa kwato za shaba 2 na utavunja vipande vipande mataifa mengi.” 1 Utatoa mapato yao waliopata kwa udanganyifu kwa Bwana, 2 utajiri wao kwa Bwana wa dunia yote.
Zechariah 4:7“Wewe ni kitu gani, ee mlima mkubwa sana? Mbele ya Zerubabeli wewe utakuwa ardhi tambarare. Kisha ataweka jiwe la juu kabisa la mwisho na watu wakipiga kelele wakisema, ‘Mungu libariki! Mungu libariki!’ ”