Isaiah 44:13
Seremala hupima kwa kutumia kamba 2 na huuchora mstari kwa kalamu; 1 huchonga kwa patasi 2 na kutia alama kwa bikari. 1 Huifanyiza katika umbo la binadamu, 2 la mwanadamu katika utukufu wake wote, 2 ili iweze kukaa katika sehemu yake ya ibada ya miungu. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 31:30Sasa umeondoka kwa sababu umetamani kurudi nyumbani kwa baba yako. Lakini kwa nini umeiba miungu yangu?”
Genesis 35:2Hivyo Yakobo akawaambia watu wa nyumbani mwake pamoja na wote waliokuwa naye, “Iondoeni miungu ya kigeni ile iliyoko katikati yenu, jitakaseni na mkabadilishe nguo zenu.
Deuteronomy 4:16ili msije mkajichafua na kujitengenezea sanamu au kinyago chenye umbo lolote kama la mwanaume au mwanamke,
Deuteronomy 27:15“Alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga au mwenye kusubu sanamu, kitu ambacho ni chukizo kwa Bwana, kazi ya mikono ya fundi stadi, na kuisimamisha kwa siri.” Kisha watu wote watasema, “Amen!”
Judges 18:24Akawajibu, “Mmechukua miungu yote niliyoitengeneza, mkachukua na kuhani wangu, nanyi mkaondoka. Nimebaki na nini kingine? Mnawezaje kuniuliza, ‘Una nini wewe?’ ”
Isaiah 41:7Fundi humtia moyo sonara, 2 yeye alainishaye kwa nyundo 2 humhimiza yeye agongeaye kwenye fuawe, 1 Humwambia yeye aunganishaye, “Ni kazi njema.” 2 Naye huikaza sanamu kwa misumari ili isitikisike. 1