Isaya 50:10
Ni nani miongoni mwenu amchaye Bwana, 2 na kulitii neno la mtumishi wake? 1 Yeye atembeaye gizani, 2 yeye asiye na nuru, 1 na alitumainie jina la Bwana, 2 na amtegemee Mungu wake. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
1 Samuel 30:6Daudi alihuzunika sana kwa sababu watu walikuwa wakisemezana juu ya kumpiga kwa mawe. Kila mmoja alikuwa na uchungu rohoni kwa sababu ya wanawe na binti zake. Lakini Daudi akajitia nguvu katika Bwana, Mungu wake.
1 Chronicles 5:20Walisaidiwa katika kupigana nao, Mungu akawatia Wahagari pamoja na wote walioungana nao mikononi mwao, kwa sababu walimlilia Mungu wakati wa vita. Alijibu maombi yao, kwa sababu walimtegemea.
2 Chronicles 20:20Asubuhi na mapema wakaondoka kuelekea Jangwa la Tekoa. Walipoanza safari, Yehoshafati akasimama akasema, “Nisikilizeni, enyi Yuda, na watu wa Yerusalemu! Mwaminini Bwana Mungu wenu, hivyo mtathibitika, wasadikini manabii wake nanyi mtafanikiwa.
Job 23:8“Lakini nikienda mashariki, hayupo; 2 nikienda magharibi, simpati. 1
Psalms 23:4Hata kama nikipita katikati 2 ya bonde la uvuli wa mauti, 1 sitaogopa mabaya, 2 kwa maana wewe upo pamoja nami; 1 fimbo yako na mkongojo wako 2 vyanifariji. 1
Psalms 25:14Siri ya Bwana iko kwa wale wamchao, 2 yeye huwajulisha agano lake. 1