Isaiah 55:7
Mtu mwovu na aiache njia yake, 2 na mtu mbaya na ayaache mawazo yake. 1 Yeye na amrudie Bwana, naye atamrehemu, 2 arudi kwa Mungu wetu, kwa kuwa atamsamehe bure kabisa. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
6Mtafuteni Bwana maadamu anapatikana; 2 mwiteni maadamu yu karibu. 1
8“Kwa kuwa mawazo yangu si mawazo yenu, 2 wala njia zenu si njia zangu,” 4 asema Bwana. 1
Cross References
Genesis 6:5Bwana akaona jinsi uovu wa mwanadamu ulivyokuwa mkubwa duniani, na ya kuwa kila mwelekeo wa mawazo ya moyo wake wakati wote ulikuwa mbaya tu.
Numbers 14:18‘ Bwana si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa upendo na mwenye kusamehe dhambi na uasi. Lakini haachi kumwadhibu mwenye hatia, huadhibu watoto kwa ajili ya dhambi ya baba zao hata kizazi cha tatu na cha nne.’
2 Chronicles 15:2Akatoka ili kumlaki Asa na kumwambia, “Nisikilizeni, Asa na Yuda wote na Benyamini. Bwana yu pamoja nanyi mkiwa pamoja naye. Kama mkimtafuta, ataonekana kwenu, lakini kama mkimwacha yeye, naye atawaacha ninyi.
2 Chronicles 30:6Kwa amri ya mfalme, matarishi wakapita katika Israeli na Yuda kote wakiwa na barua kutoka kwa mfalme na kutoka kwa maafisa wake zikisema: “Watu wa Israeli, mrudieni Bwana, Mungu wa Abrahamu, Isaki na Israeli, ili naye awarudie ninyi mliosalia, mlionusurika kutoka mikononi mwa wafalme wa Ashuru.
Job 22:23Kama ukimrudia Mwenyezi, utarudishwa upya: 2 Kama ukiuondoa uovu uwe mbali na hema lako, 1
Psalms 66:18Kama ningekuwa nimeyaficha maovu moyoni mwangu, 2 Bwana asingekuwa amenisikiliza; 1